Habari

MAJERUHI ANDRES INIESTA KUIWAHI CLASICO KAMA KAWA

on

JUMAMOSI faulo mbaya kutoka kwa
Enzo Perez dhidi ya Andres Iniesta iliwarusha roho mashabiki wa shoka ambao
walihofia makubwa, lakini bahati kiungo huyo atakuwa nje kwa kati ya wiki sita
ama nane tu, muda ambao ataiwahi Clasico.
Desemba 3, tarehe iliyopangwa
kwa mechi ya kwanza kati ya Barcelona na Real Madrid msimu huu, iko wiki sita
baadae.
Baada ya kurejea Barcelona
akitokea Valencia ambako alifanyiwa vipimo zaidi, kiungo huyo, 32, anaweza
kuanza program maalum ya matibabu.
Kiujumla Iniesta atakosa mechi
saba za Barcelona, nne katika La Liga (Granada, Sevilla, Malaga, Real Sociedad)
na mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya (Manchester City na Celtic) na mechi ya
awali ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Mfalme dhidi ya Hercules.
Hata hivyo, kama Iniesta
atahitaji wiki nane kupona, atakosa mechi tano zaidi na hatacheza hadi baada ya
mapumziko ya kipindi cha Krismasi.

Mara ya mwisho Barcelona kuivaa
Real bila ya “mchawi” wao huyo ilikuwani mwaka 2011 dhidi ya Jose Mourinho
kwenyev Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako Barca walishinda 2-0 kwenye uwanja wa
Santiago Bernabeu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *