STRAIKA wa Crystal Palace, Jonathan Benteke atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu hadi minne kutokana na jeraha la goti linalomkabili.

Mbelgiji huyo mwenye umri wa mika 21 ambaye ni mdogo wake Christian Benteke, ameshiriki mechi moja akiwa na labu hiyo tangu alipojiunga nao mwezi Agosti.

Meneja Alan Pardew amesema habari kuhusiana na jeraha hilo zilikuwa za “kukasirisha” kwa klabu hiyo na hata wachezaji.


Pardew ambaye timu yake itacheza dhidi ya Everton katika mechi ya Ligi ya Premier siku ya Ijumaa, alisema: “shida ya jeraha la goti ndio shida kubwa.”
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac