MAJERUHI LIONEL MESSI AREJEA UWANJANI KWA KUTIKISA NYAVU

MSHAMBULIAJI Lionel Messi amerejea kutoka majeruhi na kutikisa nyavu wakati Barcelona ilipoishindilia kwa kipigo cha mabao 4-0 Derpotivo La Coruna.

Ushindi huo umeipaisha Barca hadi nafasi ya pili kwenye msimamo, ikizipiku timu jirani – Real Madrid na Atletico Madrid.

Rafinha alikwamisha kwenye kamba mabao mawili huku Luis Suarez akiwa kwenye orodha ya kupachika mabao, kabla ya Messi kuingia akitokea benchi na kufunga bao la nne kwa Catalan.

Messi alirejea Barcelona wiki tatu nje ya uwanja kutokana na matatizo ya mguu. Kocha Luis Enrique alimweka benchi kiungo Andres Iniesta.

Mshambuliaji Neymar angeweza kufunga bao la mapema dakika ya saba kama sio shuti lake lililotokana na krosi ya Rafinha kukosa shabaha na kugonga mwamba.

Dakika saba baadae mpira wa adhabu ndogo wa Neymar ulipaa juu kidogo ya lango la Derpotivo.


Wageni Derpotivo walikuwa wakitumia zaidi mtindo wa mashambulizi ya kushitukiza ambayo hata hivyo hayakuwasaidia.

No comments