MAJERUHI YA BEGA YAMTOA SERENA WILLIAMS MICHUANO YA "WTA"

MKALI wa tenisi, Serena Williams amejitoa kwenye michuano ya WTA kutokana na majeruhi ya bega.

Mwanadada huyo anayeshika nafasi ywanza kwa ubora duniani, amekuwa nje ya uwanja tangu alipocheza michuano ya US Open ambapo alifika hatua ya nusu fainali huku akisumbuliwa na maumivu ya goti.

Williams mwenye umri wa miaka 35, ametangaza kuwa hatokuwa miongoni mwa washiriki wa mashindano hayo ya WTA ambayo yatafanyika jijini Singapore.

“Nimesikitishwa kutoshiriki mashindano hayo ya mwaka huu,” aliema Williams.


Mrembo huyo ambaye amechukua mataji makubwa mara 22, aliikosa michuano ya WTA mwaka uliopita.

No comments