MAN CITY CHA MTOTO KWA BARCELONA …Guardiola alizwa 4-0, Messi msumari wa moto

Lionel Messi wheels away in celebration after netting for Barcelona against Manchester City in the first halfBARCELONA ni maji ya shingo kwa Manchester City. Miamba hiyo ya Hispania imeibuka na ushindi mnono wa bao 4-0 dhidi ya kocha wao zamani Pep Guardiola.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa uliochezwa Camp Nou, hadi mapumziko Barcelona walikuwa mbele 1-0 kwa bao la Lionel Messi aliyevunga dakika ya 17.

Kipa wa Manchester City Claudio Bravo aliyesajiliwa kutoka Barcelona, alilambwa kadi nyekundu dakika ya 40 baada ya kuushika mpira nje ya eneo lake.

Barcelona nao walijikuta wakiwa pungufu dakika ya 73 baada ya Jeremy Mathieu  kuzawadiwa kadi nyekundu, lakini wakati huo tayari walikuwa mbele kwa magoli 3-0 kufuatia Messi kufunga tena dakika ya 61 na 69 kabla Neymar hajatupia bao la nne dakika ya 89.

Barcelona: ter Stegen, Mascherano, Pique, Umtiti, Jordi Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Luis Suarez, Messi, Neymar. 

Man City: Bravo, Zabaleta, Otamendi, Stones, Kolarov, Gundogan, Fernandinho, Silva, Sterling, De Bruyne, Nolito. 


No comments