MAN FONGO AMVUTA KHALID CHOKORAA KWENYE SINGELI

RAPA Khalid Chokoraa wa bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” amesema wasanii watatu wa muziki wa Singeli, Man Fongo, Sholo Mwamba na Makabila ndio waliomvutia hadi akaamua kujitosa kufanya staili ya muziki wanaofanya.

Chokoraa alisema anatamani kuwashirkisha wasanii hao kwenye nyimbo zake za Singeli anazoendelea kuandaa baada ya kurudia ule wa “Kuachwa” katika mtindo huo ambao unazidi kupata umaarufu.

“Pamoja na hayo, nina neno moja kwa wasanii wa Singeli kwamba waache kutumia maneno ya mtaani katika nyimbo zao ili muziki huu usiendelee kuonekana kama wa kihuni bali utumike kuelimisha zaidi,” alisema.


Rapa huyo alisema kuwa Singeli imeshavuka mipaka kutoka uswahilini hadi kuenea mikoa yote nchini hivyo wasanii wake hawana budi kubadilika kwa kubuni vitu ambavyo vinakwenda na wakati.

No comments