Habari

MANCHESTER UNITED YAMCHEFUA ILKAY GUNDOGAN

on

KIUNGO wa Manchester City,
Ilkay Gundogan ameiita Manchester United timu isiyo na adabu kwa kitendo
ilichomfanyia Mjerumani mwenzake, Bastian Schweinsteiger.
Schweinsteiger alijiunga na Man
United akitokea Bayern Munich majira ya joto mwaka 2015 na amecheza mechi 31
katika msimu wake wa kwanza katika soka la Uingereza.
Mkongwe huyo, 32, amekosa
nafasi katika kikosi cha Jose Mourinho, hata hivyo Gundogan amebwatuka kuwa
mashetani wekundu hawajamtendea haki mshindi huyo wa Kombe la Dunia.
“Naamini kwamba Manchester
United inaweza kufaidika kwa asilimia 100 kutoka kwa Bastian Schweinsteiger,”
Gundogan aliiambia Sport Bild.
“Kama kila tunachosikia na
kusema ni kweli, naweza kusema wamemvunjia heshima, yeye si mchezai yule wa
awali, si Yule wa miaka 18 au 19.”

Klabu kadhaa zimetajwa
kuitamani huduma ya kiungo huyo mwenye uzoefu mkubwa, ikiwa ni pamoja na MLS ya
Galax ambayo ilionyesha nia ya kumsajili mwishoni mwa mwezi uliopita.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *