MARADONA AMTAKA FRANCESCO TOTTI KUKIPIGA HADI ATIMIZE MIAKA 50

NYOTA wa zamani, Diego Maradona amemtaka staa wa timu ya AS Roma, Francesco Totti kukipiga hadi afikishe miaka 50.

Maradona aliyasema hayo juzi baada ya kumtengea pande Totti lililozaa bao wakati wa mechi ya hisani iliyopigwa mjini Roma nchini Italia.

Baada ya kupachika bao hilo, mshindi huyo wa Kombe la Dunia wa mwaka 1986, alisema kuwa anavyotaka ni kuona Totti mwenye umri wa miaka 40 akiendelea kucheza kwa muongo mwingine mmoja.

“Totti kwa ujumla ni mahiri,” alisema Maradona.
“Anatakiwa acheze hadi atakaposhika miaka 50." 

"Nilishamwambia Francesco, namuombea ili asiachane na soka kwa sababu endapo atafanya hivyo itanikera hadi kufa,” aliongeza mkongwe huyo wa zamani.

No comments