MASHABIKI WAMBEZA KING CRAZY GK ANAYEOTA SHOO YA MIL 30 BONGO

KAULI iliyotolewa na King Crazy GK kwamba hawezi kufanya shoo nchini bila kulipwa dau la sh. Mil 30, imemweka kwenye kitimoto rapa huyo aliyegeukia muziki wa kuimba baada ya kupotea kwa muda mrefu.

GK ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake “Mzuri Pesa” aliyoifanya kwa kuimba, alikaririwa hivi karibuni akisema kwamba anahitaji dau hilo refu ili kufanya shoo, hivyo yeyote anayetaka kufanya nae kazi lazima awe amejikamilisha.

“Kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi lazima awe amejikamilisha kwa sababu ukiangalia wsanii wanaotoka nje ya Tanzania wakija huku wanalipwa hadi mil 100,” alisema.

Kauli hiyo imemfanya ashambuliwe vikali kwenye mitandao ya kijamii, huku badhi ya watu wakihoji kama yeye msanii aliyepotea anataka alipwe sh. Mil 30, wakati wanaotamba sasa kama kina Harmonize, Raymond, Ali Kiba na Diamond watalipwa kiasi gani?


Hata hivyo, wengine wamemsifu kwa kueleza kuwa alichokisema ni “kiki” nzuri ya kutokea.

No comments