MASHAUZI CLASSIC KUVAMIA MORO OKTOBA 28 …Dodoma Oktoba 29, Singida na Igunga nao wamo


KUNDI la Mashauzi Classic litamimina uhondo wao kwa wakazi wa mji wa Morogoro Ijumaa ya tarehe 28 mwezi huu.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Isha MMashauzi ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Kambarage ulioko kati kati ya mji wa Morogoro maeneo ya mzunguko wa (Round about) wa kwenda SUA.

Kama vile hiyo haitoshi, Isha amesema siku inayofuata, Jumamosi Oktoba 29, Mashauzi Classic watakuwa Dodoma katika ukumbi wa Perugina.

Kwa mujibu wa Isha, wakazi wa Igunga wataonja ladha ya Mashauzi Classic Jumapili Oktoba 30 kabla ya kumalizia ratiba yao Singida Mjini Jumatatu ya Oktoba 31.

No comments