MATONYA AKAMILISHA NNE MPYA AKIWA NA KUNDI LAKE LA "BLACK IMAGE"

BAADA ya kuacha kufanya maonyesho ya muziki ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuandaa kazi mpya, msanii Seif Shaaban “Matonya” amefanikiwa kukamilisha nyimbo nne mpya.

Matonya alisema kuwa akiwa na kundi lake la Black Image, amekamilisha nyimbo nne mpya ambazo ni “Nifungulie Mlango Nitoke”, “Mr. Legeza Kidogo”, “Thamani ya Mtu” na “Kikulacho.”

“Ninataka kurudisha makali yangu kama yalivyokuwa katika albamu ya "Siamini" ambayo ilinifanya niwe na mafanikio makubwa kutokana na nyimbo kali zilizokuwa katika albamu hiyo kama vile; "Anitha" na "Violeth," alisema Matonya.


Alisema kuwa alitumia muda mrefu kuandaa vibao vipya kwa ajili ya kutoa nyimbo zitakazofanya vizuri sokoni kwa sababu ya kupambana na ushindani uliopo.

No comments