MAUA SAMA ASEMA AMAEANZA KUONA MATUNDA YA MUZIKI WAKE

MSANII anayechipukia kwa kasi katika muziki wa Bongofleva, Maua Sama amesema kuwa kwa sasa ameanza kuona matunda ya muziki wake.


Nyota huyo ambaye alivumbuliwa na msanii mwenzake wa muziki wa kizazi kipya nchini, MwanaFA, alisema kuwa awali alikuwa kwenye masoko mkoani Kilimanjaro lakini sasa yupo Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli za muziki wake baada ya kutoa nyimbo mbili ambazo ni sisikii na mahaba niue kwani zinafanya vizuri kwenye chati mblimbali nchini.

"Nashukuru hivi sasa nimeanza kufaidi raha ya kuwa msanii wa Bongofleva, namshukuru pia MwanaFA aliyekigundua kipaji changu na kuamua kunipiga tafu," alisema Maua.

No comments