MBOTO WAJIA JUU WASAMBAZAJI KAZI ZA WASANII

NYOTA wa filamu za vichekesho, Haji Salum "Mboto" amewashukia wasambazaji wa kazi za wasanii zikiwamo filamu na kusema kuwa hawaiwezi kazi hiyo na awaachie wajuzi ili kukuza kipato kwa wasanii.

Alisema kuwa, tangu Bongomovi kupata umarufu mkubwa nchini wamejitokeza wasambazaji wengi wa kazi za wasanii wakiwamo hata wale wasio na uwezo wakitaka kujinufaisha tu.

Mboto amesema umefika wakati sasa kuwaambia ukweli watu wa aina kuliko kuendelea kunyamaza huku wasanii wakiwamo hata wa muziki wa wakishimndwa kufaidika kwa jasho la kazi zao.


“Wasambazaji wa kazi za wasanii ikiwamo filamu hawaiwezi kazi waachie wajuzi wakazi hiyo,” alisema Mboto.

No comments