Habari

MCHUMBA WA BAEAKAH DA PRINCE ASEMA HAITAJI “KIKI” YOYOTE… adai sura yake ni “kiki” tosha

on

MWIMBAJI wa muziki wa Kizazi
Kipya, Najma Dattan amesema hawezi kutumia “kiki” yoyote kwa ajili ya kupata
umaarufu, akidai kwamba sura yake ni “kiki” tosha.
Najma ambaye ni mchumba wa
msanii Barakah Da Prince, alisema ameamua kuweka wazi jambo hilo kufuatia
lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, zikiwemo za kudaiwa kutafuta “kiki” kwa
kuwaharibia wenzake.
“Mimi huwa sifanyi kazi kwa “kiki”
na kwa sasa chochote nitakachokisema naweza nisieleweke hivyo nimeamua bora
nikae kimya tu, lakini ukweli ni kwamba mimi mwenyewe ni “kiki” tosha,” alisema
kimwana huyo mwenye asili ya mchanganyiko ya Mhindi na Mbongo.

Alikuwa akizungumzia tofauti
ambazo zilijitokeza hivi karibuni kati yao na boyfriend wake wa zamani, Mr.
Blue aliyekuwa akiwatuhumu Najma na Barakah kwamba walitaka kumharibia ndoa
yake kwa kumzushia mambo ya uongo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *