Habari

MECHI YA LEYLA RASHID NA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI HII…ni vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”

on

NI vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”.  Ndiyo unavyoweza kusema kuelekea mpambano wa
waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi.
Onyesho hilo linasosubiriwa kwa hamu kubwa litafanyika Jumamosi ya
tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Saalam.
Bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic
ndizo zitakazosindikiza mpambano wa mahasimu hao wawili.
“Sura Surambi” ni moja ya nyimbo ambazo piga ua lazima iwe kwenye ratiba
ya Isha Mashauzi wakati iwe isiwe Leyla naye lazima aidumbukize ngoma yake ya
“Nina Moyo Sio Jiwe” katika orodha ya nyimbo atakazotumbuiza.
Tangu onyesho hilo litangazwe, waimbaji hao wameingia kwenye vita
vikubwa vya maneno ambapo kila mmoja amejinasibu kuibuka na ushindi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *