MIRALEM PJANIC ADHIHIRISHA KUTAKA KUSEPA JUVENTUS ILI ATUE MAN CITY

MIRALEM Pjanic tayari ameonyesha azma ya kutaka kuondoka Juventus ili akatafute maisha mbele ya safari katika usajili huu wa majira ya kiangazi.

Tena amekwenda mbali zaidi kwa kutaja timu anayopenda kwenda kukipiga na kwamba mapenzi yake ni kuva uzi wa Manchester City.

Kiungo huyo ameuomba uongozi wa klabu ya Juve licha ya kumruhusu aondoke, anataka kwenda kutimiza azma yake ya kucheza Ligi ya primier.

Pjanic ambaye msimu huu amekuwa katika kiwango bora akiwa Juve, ameweka bayana ndoto yake ya kucheza katika Ligi iliyo na mashabiki wengi.

“Nina malengo ya kutimiza ndoto ya kwenda kucheza katika Ligi ya primier.”

“Ninataka kuona ninalinda kipaji changu, sitaki kuwa msiri juu ya mimi kuondoka hapa.”

“Soka ni kazi ninayokwenda kuifanya popote, ni mchezo wa kupangilia leo na kesho. Huu ndo msimamo wangu kwa sasa,” alisema Pjanic.


Manchester City ni klabu ninayoipenda kwa ajili ya soka langu la baadae. Ninaamini nina nafasi ya kucheza nikiwa kule na kutimiza ndoto yangu hii,” alisema Pjanic.

No comments