MKUU WA MAREFA AKOSOA UTEUZI WA REFA MECHI YA MAN UNITED DHIDI YA LIVERPOOL

MKUU wa zamani wa Marefu Uingereza, Keith Hackett amekosoa uteuzi wa refa kutoka Manchester, Anthony Taylo kuwa mwamuzi wa mechi ya Ligi Kuu kati ya Liverpool na Manchester United.

Taylor anaishi maili sita kutoka Old Traffoird na  Hackett anaamini huenda hilo likasababisha madai ya kupendelea upande mmoja.

“Hakuna anayetilia sana uadilifu wake,” Hackett alisema.
“Lakini je kitu kikienda mrama itakuwa vigumu kwa baadhi kuvumilia.”

Taylor hana uhusiano wowote na United lakini hushabikia klabu ya Ligi ya Taifa ya kaskazini ya Altrinvcham.


Hackett anasema inashangaza ikizingatiwa kwamba Mark Clattenburg angepatikana siku hiyo ya Jumatatu.

No comments