MNIGERIA THEOPHILUS SOLOMON KUTUA SPORTING LISBON

STRAIKA raia wa Nigeria anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya HNK Rijeka ya Croatia, Theophilus Solomon amehusishwa kuhamia katika klabu ya Spoting Lisbon ya Ureno.

Kama vile haitoshi, klabu ya Hamburg ya Ujerumani nayo imesema kwamba inahitaji bado huduma ya straika huyo ambaye amefunga mabao manne katika michezo sita ambayo amecheza.

Mchezaji huyo anadaiwa kwamba amechoshwa na maisha ya Croatia na anataka kubadili upepo huku kivutio chake kikubwa kikiwa Ureno.

Mtandao wa Owngoalnigeria.com umeandika kwamba mkataba wa mchezaji huyo na Rijeka umekoma na kwamba klabu ya Spoting Lisbon imekuwa ya kwanza kutaka huduma ya mwanasoka huyo mwenye uwezo mkubwa wa kupachika mabao.


Lakini wakati timu hiyo ya Ureno ikiwa imeshatuma posho maalum kwa mchezaji huyo, habari nyingine ni kwamba klabu ya Hamburg ya Ujerumani mwishoni mwa wiki hii itatuma watu wake maalum kwenda kumalizana na Rijeka.

No comments