MONTPELLIER YAMSAJILI MSHAMBULIAJI STEPHANE SESSEGNON WA WEST BROMWICH

KLABU ya Montpellier inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa (Ligue 1) imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa West Bromwich Albion, Stephane Sessegnon.

Montpellier wamekamilisha mpango wa usajili wa kiungo huyo kutoka nchini Benin kwa mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, ameelekea nchini Ufaransa akiwa mchezaji huru kufuatia kuachwa na klabu ya West Brom mwishoni mwa msimu uliopita.


Hii si mara ya kwanza kwa Sessegnon kuwa sehemu ya wachezaji wa klabu za nchini Ufaransa, kwani aliwahi kufanya hivyo akiwa na Paris Saint-Germain kabla hajatimkia Uingereza kujiunga na Sunderland na baadae alikwenda West Brom.

No comments