MOURINHO AMKINGIA KIFUA POGBA AKISEMA "MTAMPENDA TU MDOGO MDOGO"

MASHABIKI wa Masnchester United hawajaridhika na kazi anayoifnya kiungo wao ghali kabisa Paul Pogba, wengi wakisema ni kama “wameliwa”.

Pogba ambaye amerejea Man United akitokea Juventus ya Italia hawajavutia mashabiki wengi licha ya kwamba hajafanya vibaya sana pia.

Juzi meneja wa Manchester United Jose Mourinho amemkingia kifua akisema kwamba mashabiki wa Man United wasiwe na haraka na badala yake wampe kiungo huyo muda.

 Mourinho amesema hakutarajia Pogba ambaye alicheza vyema sana dhidi ya Fernabenche katika Ligi ndogo ya Ulaya azoee soka ya England haraka.

Amesema mchezaji huyo anafaa kuwepo muda kuzoea kucheza tena England badala ya kukosolewa kila mara.

Pogba, 23, aliyenunuliwa mwezi Agosti na kuvunja rekodi ya dunia, alifunga mabao mawili Alhamisi wakati wa ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Fernabenche.

Hata hivyo hakunga’aa Jumatatu dhidi ya Liverpool, mechi waliyotoka sare ya 0-0.

“Siku mbili zilizopita alitajwa kuwa mchezaji mbaya zaidi katika Ligi ya Premia na saa 48 anasifiwa sana,” amesema Mourinho.

“Alikuwa Italia nafahamu sifa za soka huko, kasi yake na ukali wake,” Mourinho,53, alisema.


“Kuwa Italia kwa miaka minne au mitano na kisha urejee Ligi ya Premia, sikumtarajia aanze mara moja kung’aa.

No comments