Habari

MOURINHO ASEMA BENCHI LITAWAHUSU POBGA NA IBRAHIMOVIC

on

Pogba has had a difficult start to his second spell at Old Trafford following his record move
KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amesisitiza kuwa hakuna kitakachomzuia kuwapiga benchi Paul Pobga na Zlatan Ibrahimovic pale itakapobidi.
Mourinho asema hakuna mchezaji ambaye hagusiki (untouchable) na kwamba kitu pekee ambacho hakigusiki ndani ya Manchester United ni uwajibikaji, kujituma kwaajili ya klabu na kuheshimu mashabiki.
Wachezaji hao wawili wenye majina makubwa, walicheza chini ya kiwango kwenye mchezo wa sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool, matokeo yaliyokiacha kikosi cha Mourinho kielee kwenye nafasi ya saba katika msimamo wa Premier League.
Pobga bado hajaonyesha makali yake tangu asajiliwe kwa pauni milioni 89 kutoka Juventus na hadi sasa amebahatika kufunga goli moja tu.
Ibrahimovic yeye alianza kwa makeke na kugunga mabao matano katika mechi zake tano za mwanzo, lakini amefunga mara moja tu kwenye mechi saba za mwisho. 
Mourinho says he's have no problem dropping big name players like Pogba or Ibrahimovic

Mourinho amepiga mkwara kwa Pogba na Ibrahimovic

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *