MSAGASUMU ADAI YEYE NDIYE MWANZILISHI WA SINGELI BONGO

MWIMBAJI  nguli wa muziki wa Singeli, Suleiman Jabir "Msagasumu" amedai kuwa yeye ndiye mwanzilishi  wa muziki huo hapa nchini.

“Mimi ndiye mwanzilishi wa Singeli nimeipigania sana toka enzi za vigodoro kabla havijapigwa marufuku. Nilikuwa naloop beat za taarabu hadi akina Mzee Yussuf walitaka kunishitaki, nimepigana hadi leo hii imefikia hapa,” amekimbia kipindi cha "Friday Night Live" cha EATV.

“Nilikuwa nikipata kazi nashirikisha wanangu kibao ili na wao waonekane. Kwa mara ya kwanza mimi ndiye niliyemtambulisha Sholo Mwamba, nilikuwa na kazi fulani nikampigia simu nikampa nafasi akashika kipaza akafanya mambo na watu wakaanza kumjua,” ameongeza.


Mwiumbaji huyo ameachia video ya wimbo wake  mpya wa “Iga Tena” ambao amedai kuwa wimbo huo hajamlenga mtu yeyote.

No comments