MSAGASUMU ASEMA HANA MUDA WA KUENDEKEZA BIFU ZA WASANII WENZAKE WA SINGELI

SULEIMAN Jabir “Msaga Sumu” amesema kuwa hajali bifu ambazo wasanii wenzake wa muziki wa Singeli wanamfanyia kwavile haamini katika bifu bali yeye ni kazi tu.

“Huwezi kuamini, bifu na mimi wameanza siku nyingi. Wapo wengi hao watoto, lakini naweza kuwaambia bifu na mimi watashindwa kwasababu mimi ni mtu ambaye naangalia maisha kuliko bifu,” alisema.

Alisema, wanaotafuta bifu kwake wanasaidia kumweka juu kwa madai kwamba kila anapotoa kazi wao wanafuata hichohicho kwavile hawana ubunifu kama alionao ambao umechangia kuufanya muziki wa vigodoro na mnanda kupata umaarufu.


“Mimi ninaangalia alama za nyakati. Nangalia muziki unaelekea wapi na sitaki ufalme wala nini na kama wapo waliotangulia sitaangalia walianzia na ladha gani. Mimi naimba Singeli hivyo sitaangalia anachokifanya mtu mwingine yeyote.”

No comments