MWANAMASUMBWI TYSON FURY ATANGAZA KUSTAAFU NDONDI

BINGWA wa ndondi katika uzani mzito duniani, Tyson Fury amesema kuwa amejiluzulu mchezo huo katika ujumbe uliochapishwa katika mtandao wa Twitter.

Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 alijiondoa katika pigano la marudio dhidi ya raia wa Ukrain, Wladmir Klitschko lililopangwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu kutokana na masuala ya kiafya.

Fury ambaye anamiliki mataji ya WBA na WBO, anakabiliwa na kesi mnamo mwezi Novemba inayohusisha madai ya utumiaji wa madawa ya kusisimua misuli.

“Ndondi ni kitu kibaya zaidi nilichoshiriki,” alisema kupitia mtandao wake wa Twitter akiongezea: “Mimi ndiye bingwa na aliyestaafu.”

Fury alitarajiwa kupata kitita kikubwa tangu alipojiunga na ndondi wakati wa pigano lake la pili dhidi ya Klitschko katika uwanja wa Manchester mwezi huu.


Amepewa siku kumi 10 na shirikisho la ndundi WBO kutoa maelezo na kuahirishwa kwa pambano lake hilo la marudio kwa mara ya pili.

No comments