MWANAMIELEKA JAMES HELLWIG AFARIKI DUNIA WIKI ILIYOPITA

MKONGWE wa mieleka ulimwenguni, James Hellwig “Ultimate Warrior” amefariki dunia mwanzoni mwa juma lililopita baada ya kutoa hutuba nzuri katika usiku wa Raw.

Shirikisho la mieleka (WWE), lilithibitisha kifo cha nyota huyo katika tovuti yake: “WWE imeshitushwa na kuhuzunishwa na taarifa za mkongwe huyu wa WWE Superstars.”

Mwanamieleka huyo alianza medani hiyo mwaka 1987 na kwa haraka sana akawa ni miongoni mwa nyota wakubwa katika historia ya WWE.


Warrior alitwaa ubingwa WWE kule Wrestle Mania VI baada ya kumzabua Hulk Hogan katika pambano lililovuta hisia za mashabiki wengi.

No comments