…NA HUU NDIO WIMBO WA ISHA MASHAUZI UNAOMVUTIA LEYLA MASHAUZI

MALKIA wa mipasho kutoka Jahazi Modern Taarab, Leyla Rashid ameshindwa kuficha hisia zake pale alipoamua kuweka wazi kuwa akipenda zaidi kibao cha mwimbaji wa Mashauzi Clasic Modern Taarab, Isha Mashauzi, “Ya Wenzenu Midomoni”.

Katika kuthibitisha hilo aliloliongea ndani ya Studio za Radio Free Afrika, katika kipindi cha “Kona ya Mwambao”, Leyla aliiimba kwa ufasaha sehemu ya kibao hicho kilichomo kwenye albamu ya kwanza ya Jahazi Modern Taarab, “VIP"

Leo hii baadae, Leyla na Isha watakutana uso kwa uso, kwenye pambano kali lililoandaliwa maalum kwa ajili yao, ndani ya Darlive, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam ambapo kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

No comments