NAY WA MITEGO AKANA KUWA NA BIFU NA BARAKA DA PRINCE

MSANII Emanuel Elibariki “Nay wa Mitego” amesema hana bifu na msanii yeyote yule akiwemo Baraka Da Prince.

Akizungumza jijini Dar es Salam hivi karibuni, Nay amesema anashangazwa na Baraka kumtolea maneno ya kashfa na kumwita msanii wa kuungaunga.


Mwanzoni mwa wiki hii Baraka Da Prince amesikika akimtuhumu Nay kuwa ni msanii wa kuungaunga na kazi yake kubwa niu kudhalilisha wanawake kwa kuwapiga picha za ovyo.

No comments