RAPA asiyeishiwa vituko, Nay wa Mitego amesema anapoamua “kuwachana” wasanii wenzake huwa hatafuti “kiki” bali anafanya jambo ambalo ana uhakika nalo kwa asilimia 100.

Alisema, wapo watu ambao wamekuwa wakimponda kwa kusema anatafuta “kiki” na kufafanua kwamba hilo halina ukweli wowote kwavile alishapata umaarufu miaka mingi na bado anaendelea kuupata.

“Nilishagundua kwenye muziki wa Bongofleva siku hizi kuna wasanii wengi maboya ambao wanatakiwa kuambiwa ukweli, lakini ajabu ni kwamba nikiusema ninaambiwa ninatafuta “kiki”,” alisema.


Rapa huyo alisema kuwa mwanzo walikuwepo wachache lakini sasa amegundua wapo wengi na wapo wanaomwona yeye kama boya ila uboya wake una faida na kwamba lazima awachane katika nyimbo zake.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac