NAY WA MITEGO: UKWELI WA "KUWACHANA" WASANII WENZANGU UNANIWEKA HURU

RAPA Nay wa Mitego amesema ukweli unamweka huru na hataacha kusema hata kama kuna watu wanaoumia kutokana na ujumbe anaoufikisha kupitia nyimbo zake.    

“Kwa kawaida yangu kama nina uhakika kuwa kuna msanii ama mtu yeyote anafanya jambo ambalo ninaamini halina manufaa kwa umma, huwa ninamsema bila woga kwa sababu ukweli unaniweka huru,” alisema Nay wa Mitego.

Alisema kuwa, katika mazingira hayo lazima achukiwe lakini ataendelea kusema ukweli kwa njia ya muziki akiamini dawa chungu ndio inayoponyesha.

Nay wa Mitego alisema kuwa anachukiwa na watu wasiopenda kuambiwa ukweli na ndio hao pia ambao wamekuwa wakimtukana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Hata hivi karibuni nilitukanwa na msanii mmoja mchanga kwa sababu tu ya kusimamia ukweli, lakini nirudie tena kwamba ukweli unanifanya niwe huru ndio maana siogopi,” alisema.

No comments