NEW AUDIO: "MAPUNGUFU YANGU" KETE YA KWANZA YA IVORY BAND ...utunzi wake Dogo RamaHATIMAYE Ivory Band wamedumbukiza sokoni kete yao ya kwanza kabisa kupitia wimbo “Mapungufu Yangu”.

Tangu ianzishwe miezi kadhaa iliyopita, Ivory Band ilikuwa haijaachia hewani wimbo wowote, lakini sasa wanafungua kabati lao na kuachia kigongo kimoja kitamu.

Huu ni utunzi wake Dogo Rama, kazi aliyoanza nayo katika bendi ya Double M Plus kabla yeye na wenzake hawaondoka na kuanzisha Ivory Band na kuhama na wimbo wake huu.

Isikilize kazi hii nzuri ya Ivory Band yenye urefu wa dakika nne na sekunde nne ambapo ndani yake utasikia sauti yake Dogo Rama, Saleh Kupaza, Amina Juma na Rama Pentagon.

No comments