NEW AUDIO: “MAUMIVU” RUMBA LAINI KUTOKA KWA 33
MULOMBA TSHILUMBA mwimbaji mwenye sauti matata kupitia muziki wa dansi, akijulikana zaidi kama 33, anashuka na kitu kikali kinachokwenda kwa jina la “Maumivu”.

Ni 33 yule yule aliyetingisha anga ya muziki wa dansi kupitia wimbo “Moyo Wangu” akiwa na kundi la FM Academia “Wazee wa Ngwasuma”.

Lakini safari hii 33 anakuja kivyake vyake, hii ni kazi yake binafsi ambayo itakupa burudani mwanana kupitia rumba laini mithili ya ute wa yai.

Isikilize hapo juu kazi hiyo ya 33 itakayokudhihirishia kuwa kazi bora za muziki wa dansi zipo.

No comments