NI VITA YA KISASI KATI YA JOSE MOURINHO NA JURGEN KLOPP LEO

UTAMU wa Ligi Kuu ya England unazidi kunoga wakati leo vijogoo wa Anfield Liverpool watakapokuwa kwenye dimba lao la nyumbani kuwakaribisha Manchester United.
Mchezo huo utapigwa majira ya 4:00 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.

Mchezo huo umevuta hisia kubwa za mashabiki wa soka hasa upinzani uliopo kati ya makocha wake, Jurgen Klopp na Liverpool na Jose Mourinho wa Manchester United.

Mourinho anakabiliwa na changamoto ya kufanya maamuzi kama atamwacha benchi mshambuliaji wake, Wayne Rooney kwenye mchezo huo au kumweka katika kikosi cha kwanza.

Rooney amekuwa na wakati mgumu zaidi katika wiki za hivi karibuni baada ya kuachwa kwenye kikosi cha kwanza cha Man United na kile cha timu ya taifa ya England.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesababisha mgongano wa mawazo kwa wachambuzi wa soka, huku wengine wakitaka atumike kama kiungo badala ya kuendelea kumchezesha kama mshambuliaji.

Rooney amejikuta akipata watetezi wakati mshambuliaji wa zamani wa Man United, Dwight Yorke akibainisha wazi kwamba nyota huyo bado yupo fiti kuendelea kuibeba United.

“Watu kwenye soka huwa wanasahau mapema, ameisaidia timu kwa muda mrefu rakini wote wamesahau mabao yake. Rooney bado ana uwezo wa kuendelea kucheza.”
Kwa upande wake kocha Mourinho ameuzungumzia mchezo huo kwa kuufananisha na ule wa El Classico unaozikutanisha Real Madrid na Barcelona kwenye Ligi Kuu ya Hispania.

“Ni mchezo mgumu, Liverpool wameanza vizuri Ligi Kuu, hivyo kwa namna yoyote ile tutakuwa na changemoto kubwa kuwakabili,” amesema Mourinho akizungumza na BBC Sport.
“Baada ya dakika 90 kila kitu kitakuwa wazi kwa sasa wacha tusubiri kitakachotokea uwanjani.”

Kwa upande wake kocha Klopp anaamini kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini ana imani kubwa na kikosi chake.

“Tumeanza vizuri kwenye mechi za Ligi Kuu msimu huu, nawaamini wachezaji wangu lakini kikubwa ni kwamba tunaingia mchezoni kwa kazi moja tu, kuhakikisha tunapata pointi zote tatu,” amesema Klopp wakati akizungumza na Daily Mail.

Liverpool ilipoteza mechi zake nne zilizopita za Ligi walipokutana na United na sasa wana nafasi nzuri ya kulipiza kisasi.

Liverpool imeshinda mechi zake mechi zake nne mechi zake nne mfululizo zilizopita za Ligi Kuu na kuweza kujivuta hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.


Wakati mchezo huo ukiwa umeteka hisia za wengi, mkuu wa zamani wa maamuzi Uingereza, Keith Hackett amekosoa uteuzi wa mwamuzi jiji la Manchester, Anthony Taylor kuchezesha mchezo huo.

No comments