ODAMA ASEMA KUJIFICHA NA KUIBUKA NDIO STAILI YAKE ANAPOTAKA KUTOA KAZI MPYA

NYOTA wa Bongomuvi, Jenifer Kyaka “Odama” amesema anapenda kujificha kiasi kwamba hadi watu huuliza yuko wapi, lakini hiyo ndio staili yake kuelekea kutoa kazi mpya.

Alisema kazi ya kuandaa filamu sio ya kulipua tu bali msanii anatakiwa kutuliza kichwa na kuangalia soko linakwendaje na pia kuangalia wasanii wanataka nini.

“Hilo ni la muhimu sana katika filamu na mimi huwa nafanya hivyo hadi watu wanajiuliza niko wapi bila kujua kwamba ninajipa muda wa kutosha ili niandae vitu vinavyowakuna mashabiki,” alisema Odama.


Alisema kuwa ana kawaida ya kujipa muda wa kutosha katika maandalizi zake, ndio maana tangu kuanza kwa mwaka huu alitoa filamu ya “Mkwe” na sasa anakuja na nyingine ambayo ataitaja jina wakati mwafaka ukiwadia.

No comments