MWANAMUZIKI nguli wa dansi Nguza Vicking “Babu Seya” na mwanaye Papy Kocha ambao wanatumikia kifungo gereza la Ukonga, watapanda jukwaani Ijumaa hii na kumwaga uhondo ‘live’ kwa wafungwa wenzao.

Hiyo ni katika tamasha maalum la wafungwa lililoandaliwa na Global Publishers katika kuadhimisha siku ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere – “Nyerere Day”.

Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo ameithibirtishia Saluti5 kuwa vibali na taratibu zote za shughuli hiyo itakayofanyika ndani ya gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, zimekamilika.

Mbizo amesema mbali ya Papy na Nguza kutumbuiza, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa The African Stars “Twanga Pepeta” na Msagasumu.

Kwa mujibu wa mbizo, tamasha hilo litakuwa na michezo mbali mbali kwa wafungwa kama vile mechi za mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbia na magunia, pamoja na kuimba na kurap ambapo zawadi mbali mbali zitatolewa kwa washindi.


NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac