PATRICE EVRA, LUIS SUAREZ WAMALIZA TOFAUTI ZAO

PATRICE Evra na Luis Suarez ni wachezaji waliokuwa na uadui mkubwa wakati wakicheza EPL kutokana na mitafaruku iliyokuwa ikitokea kati yao.

Mashabiki wa soka watakumbuka kwamba Luis Suarez aliwahi kumtolea maneno ya kibaguzi Evra wakati wakiwa Manchestrer United na Suarez akicheza Liverpool, Suarez tena akakataa kusalimiana na Evra wakati timu hizo zilipokuwa zikikutana kwenye mchezo wa EPL.

Mgogoro wao umedumu kwa muda mrefu hata wakati huu ambapo kila mmoja ancheza kwenye Ligi tofauti, Evra akicheza Juventus ya nchini Italia huku Suarez akicheza Barcelona ya Hispamnia.

Lakini Evra kwa kuonyesha ukomavu wake wa akili ameamua kuachana na hali hiyo na kufuata njia nzuri ya kuishi kwa amani na Suarez.

Evra amesema hataki tena kuishi na aina hiyo ya maisha dhidi ya Suarez na kumpongeza kwa kushinda tuzo ya mfungaji bora wa La Liga na kupata kiatu cha dhahabu.


Ameandika hivi: “Kwenye Instagram kuna maneno upendo tu na hakuna neno chuki. Luis wewe ni mchezaji mkubwa na bora sana, wewe ni namba tisa bora. Hongera sana Luis, Luis Suarez 9. Naupenda sana huu mchezo hahahah.”

No comments