PAUL MERSON AMSHUSHA POGBA NA KUMPANDISHA JORDAN HENDERSON

NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya England, Paul Merson ambaye sasa ni mchambuzi wa soka, amesema kwake ni sahihi kuwa na mchezaji kama Jordan Henderson kuliko Paul Pogba.

Merson anadai kwamba Henderson, kiungo wa Liverpool ndiye bora zaidi.

Wachezaji hao wanatarajiwa kusuguana katika mechi kali ya mahasimu wa Ligi Kuu England kwenye uwanja wa Anfield kesho, wakati Jose Mourinho atakapoipeleka Reds kwenye uwanja huo.

Henderson amekuwa na msimu mzuri akifunga bao tamu kwenye mechi dhidi ya Chelsea, lakini pia akivaa kitambaa cha unaodha wakati England ilipotoka sare dhidi ya Slovenia.

Alipoulizwa kuhusu kiungo gani anayemchengua kwenye timu yake, Merson alisema:

“Leo ni Jordan Henderson kama utaniuliza nimchague nani.”
“Miaka 10 ijayo sijui labda inawezekana wakajiuliza kiasi gani cha fedha wametumia kwa Pogba.”


“Henderson amekuwa kwenye kiwango kizuri Ligi Kuu kulinganisha na Pogba ambaye bado hajaonyesha ubora wake.”

No comments