PAUL POGBA AMCHEFUA JOSE MOURINHO

KIMENUKA. Kiungo wa bei mbaya Manchester United, Paul Pogba tayari ameshamkera kocha wake, Jose Mourinho kutokana na kiwango “dhaifu” alichokionyesha katika mechi ya sare ya bila kufungana na Liverpool usiku wa kuamkia Jumanne kwenye uwanja wa Anfield.

Mashetani wekundu walicheza vizuri kwenye safu ya ulinzi na kuzuia safu hatari ya ushambuliaji ya Liverpool kupata bao katika mechi hiyo.

Mourinho amemshutumu kiungo huyo akisema alikuwa tatizo sambamba na straika Zlatan Ibrahimovic aliyeshindwa kuusukumiza kwenye kamba mpira kwa kichwa katikati ya kipindi cha pili.

“Ingekuwa bao 1-0 na mchezo ungemalizika,” alisema Mourinho wakati akizungumza na Sky Sports. “Nilitegemea makubwa zaidi kutoka kwa Pogba, sikuridhika na alivyocheza.”


“Safu ya ulinzi ilifanya kazi nzuri. Tulikuwa na nafasi nzuri ya kufunga, nilidhani Zlatan angefunga bao.”

No comments