PEP GUARDIOLA AGOMA KUBADILI MFUMO WAKE

LICHA ya kocha wa Manchester City, Pep Guardiola kupokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya timu yake ya zamani ya Barcelona katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, amedai kuwa hana mpango wa kubadilisha mfumo wake.

Katika mchezo huo, Lionel Messi ambaye alikuwa ni mchezaji wake tegemeo wakati kocha huyo yupo Barcelona, lakini kwenye mchezo huo Messi alionyesha uwezo wake na kumdhalilisha kocha huyo huku mshambuliaji huyo akiondoka na mpira baada ya kufunga mabao matatu peke yake na bao la nne likifungwa na Neymar.

Kutokana na Guardiola kushindwa kutamba kwenye uwanja huo wa Nou Camp, amedai kuwa japokuwa amepoteza mchezo huo lakini hawezi kubadilisha mfumo wake na anaamini ataleta changamoto nchini England.

“Naweza kusema kwamba mifumo ambayo ninaitumia katika soka nitaendelea kufanya hivyohivyo hadi mwisho wangu wa kufundisha, siwezi kubadilisha na sina mpango huo hata kama timu inapoteza mchezo wake.”


“Mfumo ambao tunautumia na kupata matokeo mazuri ni huohuo ambao katika baadhi ya michezo tunapoteza, siwezi kubadilisha kutokana na kupoteza baadhi ya michezo wakati ipo michezo mingi ambayo tunafanya vizuri.”

No comments