Habari

PEP GUARDIOLA APONDA STAILI YA MIPIRA MIREFU YA MANCHESTER UNITED

on

PEP Guardiola ameponda staili
ya Manchester United ya kutumia mipira mirefu wakati akifafanua anachotaka
kukiona kwa timu yake ya Manchester City.
City walilala 1-0 Old Trafford
katika mechi ya EFL katikati ya wiki na ikaelezwa kwa Guardiola kwamba timu
yake ilishindwa kucheza kwa staili yao kutokana na ukabaji wa kutumia kasi
kubwa wa United.
 Guardiola hakulichukulia poa jambo hilo
akisisitiza kwamba timu yake inaweza kucheza soka mbele kwa mbele lakini kikosi
cha Jose Mourinho kimeshindwa kutokana na kupiga mipira mirefu juu, staili
ambayo yeye kamwe hataitumia.
“Dhamira ya United ilikuwa ni
mpira mrefu. Ukipoteza mpira unapogombea kwa hewani wanakufunga goli,” alisema.

“Wakati mwingine unafungwa goli
kwa sababu unalazimika kuanza kujenga mashambulizi kama haya. Na wakati
mwingine unapiga mipira mirefu na unafungwa pia.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *