PEP GUARDIOLA APONDWA NA KOCHA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Vanderilei Luxemburgo ameibuka na kumponda kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akidai kuwa Mhispania huyo ni mzuri zaidi kwenye soko la usajili na sio ufundishaji soka.

Luxemburgo anaamini kuwa Guardiola hastahili sifa anazopewa na kwa upande wake Carlo Ancelotti ndiye kocha bora ulimwenguni.

“Alijizolea umaarufu mkubwa akiwa Barcelona lakini Luis Enrique  amekifanya alicho kifanya yeye,” alisema Luxemburgo.

No comments