Habari

PICHA 15 ZA MSONDO NGOMA WALIVYOWEKA HESHIMA MANGO GARDEN

on

Msondo Ngoma Music Band wamedhihirsha kuwa hawabahatishi pale
linapokuja suala la lile tamasha lao la Msondo Family Day linalofanyika kila
wikiendi ya mwisho wa mwezi.
Ijumaa iliyopita Msondo walifanya tamasha hilo ndani ya ukumbi wa
Mango Garden Kinondoni na kujaza mashabiki wengi wa muziki wa dansi.
Msondo wakangurumisha bonge la burudani lililokuwa na mseto mtamu wa
nyimbo zao za zamani sana, zamani kiasi hadi zile mpya kabisa.
Moja ya nyimbo za zamani zilizotia fora sana ni “Sogea Karibu” wa
mwaka 1980 utunzi wake Belesa Kakere huku miongoni mwa nyimbo mpya kabisa
zilizotesa ni “Masimango” utunzi wa Edo Sanga.
 Wakali wa muziki wa dansi kutoka Clouds FM …Khamis Dacota (kushoto) na Dj Bulla
Shaaban Dede
 Edo Sanga
 Hassan Moshi 
 Mashabiki wa Msondo katika ubora wao
 Tazama nyomi la Msondo
 Seneta wa Msondo Abdulfareed Hussein na Dj Bulla
 Pangamawe katika mpini wa solo
 Pishuu akikamua kiulani gitaa la kati
 Mtangazaji Sofia Rajab wa Capital Radio akisalimia mashabiki
 Kundi la kina mama mashabiki damu wa Msondo Ngoma
 Zahoro Bangwe “Kidevu Cheupe”
 Zawadi ya saa ikitolewa kwa shabiki wa Msondo
MC alikuwa ni Rajab Zomboko kutoka Radio One na ITV

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *