PICHA 4: ISHA MASHAUZI ALIVYONGURUMA TIMES FM JUU YA LEYLA RASHID …unajua alichojibu Leyla?


ALHAMISI mchana Isha Mashauzi aliitwa Times FM kupitia kipindi cha Mitikisiko ya Pwani ambapo kubwa aliloitiwa ni juu ya mpambano wake na malkia Leyla Rashid wa Jahazi Modern Taarab.

Isha akatumia nafasi hiyo kujinadi na kueleza namna atakavyomfunika Leyla Rashid.

Waimbaji hao wawili watapambana Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live huku wakisindikizwa na Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic.

Mwimbaji huyo, boss wa Mashauzi Classic akasema kitu cha kwanza anachojivunia ni uwezo wake wa kuweza kusimama jukwaani kwa masaa matatu mfululizo, kitu alichodai kuwa sio Leyla tu bali hakuna mwimbaji yeyote wa taarab mwenye pumzi hizo.

“Nina uwezo wa kusima jukwaani kwa masaa matatu mfululizo, nikaimba na kwa ubora ule ule, kwa hili ni mtihani mzito kwa Leyla, hana pumzi za kusimama jukwaa moja na mimi,” alitamba Isha.

Mkali huyo akasema yeye ndiye malkia wa masauti matamu, ana sauti zaidi ya 18 wakati Leyla ana sauti moja.

Mtangazaji wa Times FM anayehost kipindi hicho cha Mitikisiko ya Pwani, Dida akawaahidi wasikilizaji kuwa Alhamisi ijayo Leyla atakuwa kikaangoni live ili na yeye aweze kujibu mapigo ya Isha, halafu baadae wote wawili (Isha na Leyla) watapewa fursa ya kupeana makavu uso kwa uso hapo hapo Times FM kupitia Mitikisiko siku hiyo ya Alhamisi …siku mbili kabla ya mpambano wao.

Leyla alipoulizwa na Saluti5 juu ya majigambo ya Isha, akasema kikazi Isha ni mtoto mdogo kwake.

“Sina chochote ninachohofia kwa Isha Mashauzi. Isha ni wa juzi na bado hajaiva, udhaifu wake naujua mimi, ataumbuka Dar Live,” alisema Leyla.
 Isha akiwa ndani ya studio za Times FM Alhamisi iliyopita
 Mtangazaji wa Times FM, Dida akitupia maswali yake ya uchokozi
 Isha akipiga mkwara mzito
Dida na Isha


No comments