PICHA 4 ZA KILICHOTOKEA RFA: ISHA NA LEYLA WAZUNGUMZIA BIFU LAO NDANI YA JAHAZI


WAIMBAJI nyota wa taarab watakaopambana leo usiku katika ukumbi wa Dar Live, Isha Mashauzi na Leyla Rashid, jana walizungumzia kile kinachotajwa kuwa wana bifu kubwa lililoanzia Jahazi Modern Taarab.

Lakini waimbaji hao wakiongea na kipindi cha "Kona ya Mwambao" cha Radio Free Africa, wakasema katu hawakuwahi kuwa na bifu.

“Sikuwahi kuwa na bifu na Leyla na si kweli kuwa niliondoka Jahazi eti kwa sababu nilikuwa na ugomvi na Leyla, mimi niliondoka Jahazi ili kusaka changamoto nyingine za kisanii,” alisema Isha.

Kwa upande wake Leyla alikuwa na haya ya kusema: “Sijawahi kugombana na Isha na wala hakunivunjia heshima hata siku moja. Kama Isha ni mkorofi basi labda kwa wengine lakini mimi hajawahi kunikorofisha.”

Wasanii hao wakafafanua kuwa kinachotokea ni upinzani wa kikazi unaotiwa utambi na mashabiki wao.
 Mtangazaji wa RFA Najima akiongea na Isha
  Mtangazaji wa RFA Najima akiongea na Leyla
  Leyla, Najma na Isha katika picha ya pamoja
Najma

No comments