PICHA 6: LEYLA RASHID NA ISHA MASHAUZI WALIVYOKINUKISHA TIMES FM ALHAMISI MCHANA


MAHASIMU wawili ambao kwa sasa wanakimbiza vizuri soko la muziki wa taarab, Isha Mashauzi na Leyla Rashid, jana mchana walikinukisha ile mbaya kwenye kituo cha radio cha Times FM jijini Dar es Salaam.

Waimbaji hao ambao Jumamosi hii watakuwa na mpambano mkubwa utakaofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, waliitwa kwenye kipindi cha Mitikisiko ya Pwani ili waweze kujinasibu juu ya onyesho lao hilo la Nani Zaidi.

Isha akakiri kuwa Leyla ni amemtangulia kwenye fani lakini uwezo wake ‘umedumaa’ na kwamba atamfunika kiulani.

“Leyla amenitangulia na alinikaribisha Jahazi, lakini kikazi nimemzidi sana na ndiyo maana nimekuwa na uwezo wa kuanzisha bendi yangu, yeye bado yuko chini ya mtu,” alitamba Isha.

Naye Leyla akajibu mapigo kwa kusema Isha hana utulivu kwenye uimbaji, ana vurugu na makelele mengi.

“Isha ni mwepesi sana, anachojua yeye ni makelele na vurugu jukwaani lakini hajui kuimba,” alisema Leyla Rashid.

Waimbaji hao walizodoana sana na kunyimana pumzi, kila mtu akatamba na kumpiga vijembe mwenzake kiasi kwamba mwendeshaji wa kipindi hicho Dida akawa na kibarua kizito cha  kuwatuliza.

Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic ndiyo watakosindikiza onyesho hilo la kukata mzizi wa fitana.
 Mwaisiti Robert akishiriki kwenye mahojiano ya Isha na Leyla ndani ya  Times FM 
 Isha na Leyla ndani ya  Times FM sambamba na mtangazaji Dida wa Shaibu
 Isha akijinadi
 Leyla akitabasamu kwa dharau
 Leyla na Isha walipokutana mjengoni Times FM
Leyla akimwaga sera zake

No comments