PRINCE AMIGO APATA KIGUGUMIZI KUTAJA NANI ZAIDI KATI YA ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID …aacha fumbo kubwa


MPAMBANO wa Isha Mashauzi na Leyla Rashid ni wa moto kuliko hata moto wenyewe! Watu wanashikwa na kigugumizi pale wanapoulizwa nani mkali zaidi.

Alhamisi iliyopita mwimbaji nyota wa Jahazi Modern Taarab Aboubary Soud “Prince Amigo” alikaribishwa jukwaa la Mashauzi Classic (Mango Garden) kuzungumzia machache juu ya mpambao wa Leyla na Isha utakaofanyika Jumamosi hii ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuzungumza makubwa yanayotarajiwa kufanyika katika onyesho hilo, Amigo akatakiwa kusema ni nani zaidi kati ya Isha na Leyla na hapo ndipo ‘kigugumizi’ kilipowadia.

Amigo akasema: “Jibu langu litawaacha Dilemma (njia panda) …Sasa nimpe nani, anayejua mapenzi,” Amigo akaimba kipande cha Isha Mashauzi cha wimbo “Nimpe Nani” na kufanya ukumbi mzima ulipuke kwa furaha  wakidhani anamaanisha Isha ndiye zaidi.

Lakini Amigo akaendelea: “Tulieni! Tulieni! …Nina Moyo, sio jiwe,” hapo akaimba kipande cha Leyla na kuwapoteza maboya mashabiki.

Amigo akajaribu kufafanua: “Hawa waimbaji wote wawili ni wakali, lakini kila mtu ana muono wake na mapenzi yake kwa yule anayemkubali.

“Unaweza ukasema fulani mkali kwa vile tu upo nae sehemu moja lakini kumbe inaweza kuwa tofauti.


“Leo hii meneja Sumaragar anaweza akasema Isha mkali lakini kumbe moyoni anamkubali Leyla. Na mie Amigo ninaweza nikesema Leyla mkali lakini kumbe namkubali zaidi Isha.”

No comments