PRINCE AMIGO ASEMA YEYE NDIYE MSANII PEKEE WA KIUME ATAKAYEIPELEKA TAARAB ANGA ZA KIMATAIFA


MWIMBAJI nyota wa Jahazi Modern Taarab ambaye kwasasa ndiye nguzo kubwa ya kundi hilo, Prince Amigo, amesema yeye ndiye msanii atakayeipeleka taarab katika anga za kimataifa kwa upande wa wasanii wa kiume.

Amigo aliyasema hayo hivi karibuni katika onyesho la Jahazi lililofanyika ndani ya ukumbi wa Lunch Time Manzese jijini Dar es Salaam ambapo alisisitiza kuwa kwa sasa hakuna msanii mwingine wa kiume wa taarab hapa nchini ambaye anaweza kuipeleka taarab kwenye ‘level’ zingine zaidi yake.

“Nikiangalia kwa wasanii wa kiume taarab simuoni anayeweza kufanya makubwa kunizidi mimi, hakuna. Mimi ndiye nitakayeipeleka taarab kwenye anga za kimataifa,” alisema Amigo.

Mwimbaji huyo anayetesa na nyimbo zake kama “Domo Kaya”, “Hundred Percent”, “Full Shangwe” na “Tiba ya Mapenzi” alisema yeye kwa kushirikiana na Jahazi watafanya makubwa yatakayoshangaza wengi.

“Mimi nawaapia hapa mbele yenu, Jahazi haliwezi kuyumba, tutafanya mambo makubwa na mazuri” alitamba kwa kujiamini Amigo.

No comments