PROF JAY ASEMA NI MUHIMU MSANII KUSOMA ISHARA ZA NYAKATI KULIKO KUBWETEKA

RAPA mkongwe, Joseph haule “Prof Jay” amesema kuwa ni muhimu kwa msanii kusoma ishara za nyakati na kwenda kulingana na mazingira, badala ya kubweteka tu na kujikuta akipitwa na wakati.

Alisema kuwa yeye ameliona hilo akaamua kujitosa kwenye muziki wa Singeli ambao ila uchao unazidi kujipatia umaarufu ingawa wapo baadhi ya wasanii wameponda hatua yake hiyo.

“Baada ya kutoa wimbo wa “Kazi kazi” ulio katika mtindo wa Singeli, baadhi ya wasanii wenzangu wamenisema eti mimi sio mwana Hiphop tena, lakini niwaambie tu kuwa ni muhimu msanii kusoma ishara za nyakati,” alisema Prof Jay.


Alisema, kwa sababu muziki huo ambao awali ulikuwa kama wa watu wahuni, anataka kuhakikisha kwamba unajulikana kimataifa badala ya kuendelea kuwa wa uswahilini tu.

No comments