PROFESA JAY AWAPASHA WASANII KWENYE MUZIKI HAKUNA NJIA YA MKATO YA MAFANIKIO

RAPA mkongwe, Joseph Haule “Profesa Jay” amesema kuwa katika muziki hakuna njia ya mkato ambayo inaweza kuwafanya wasanii wakapata mafanikio zaidi ya ubora wa tungo zao.

Jay alisema kuwa bahati mbaya wasanii wengi hawajagundua hilo na sasa wamejikita zaidi kwenye kutafuta “kiki” wakidhani kwamba zitawatoa kumbe ndio zinawaharibia zaidi.

“Ukiwafuatilia wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya, utagundua kuwa asilimia kubwa wanatumia kiki ambazo sasa zinafunika hata nyimbo zao, ndio nimeona niwape ushauri kidogo,” alisema Jay.


Rapa huyo alisema Singeli imeshavuka mipaka kutoka uswahilini hadi kuenea mikoa yote nchini, hivyo wasanii wake hawana budi kubadilika kwa kubuni vitu ambavyo vinakwenda na wakati.

No comments