RAHAMA SADAU AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA UIGIZAJI NIGERIA

MWIGIZAJI mahiri wa filamu wa Nigeria, Rahama Sadau kutoka jimbo la Kano, Nigeria amefungiwa kujihusisha na uigizaji kwa muda usiojulikana.

Katika maamuzi yake ya kumfungia msanii huyo ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kutumia lugha ya Kihausa, chama kinachosimamia ubora wa picha za video nchini Nigeria (MOPPAN), kimesema msanii huyo amewakera waumini wa dini ya Kiislamu.


Rahama ameponzwa na uchezaji wake akikumbatiana na baadae kumlalia kifuani katika picha iliyosambaa kwa kasi, kitendo ambacho kinaweza kuwaletea matatizo na waumini wa dini ya Kiislamu ambao wanapinga viashiria vya kimapenzi hadharani.   

No comments