RASHFORD ASEMA ZLATAN IBRAHIMOVIC NI 'MTAJI' KWA WASHAMBULIAJI CHIPUKIZI


MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Marcus Rashford anataka kutimiza ndoto zake kupitia kwa  Zlatan Ibrahimovic akiamini kuwa ana mengi makubwa ya kujifunza kutoka kwa straika huyo mkongwe mwenye mataji kibao mkononi. 

Ibahimovic alijiunga na Manchester United akitokea Paris Saint-Germain ya Ufaransa dirisha la kiangazi  na kwa sasa Rashford anajivunia kupata nafasi ya kujifunza kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 35.

“Ni jambo la kushangaza nimepata washambuliaji wakubwa duniani ndani ya timu kama vile Zlatan na Wayne Rooney,” Rashford aliiambia tovuti ya Manchester United.

“Kwa wachezaji  chipukizi kama mimi, Anthony Martial na Jese Lingarid hatuna kitu cha kutakiwa kufanya bali tunachopaswa kuangalia ni jinsi washambuliaji hawa mashuhuri wanavyocheza na wanavyofanya  mazoezi. Huwezi kutuuliza kitu chochote."

No comments